Karibuni mabibi na mabwana!

April 3, 2006 at 12:39 am Leave a comment

Wasomaji wapendwa –
Nimetiwa moyo kuanza kublogu katika Kiswahili na kumbukumbu niliyo nayo kwa heshima ya waalimu wangu wa Kiswahili nilokuwa nao tangu darasa la kwanza hadi shule ya upili.
Hivi namshukuru marehemu Bi. Rose Okello, Bi. Akoto, Bw. Obed, Bw. Misiko na Bi. Maloba.
Kidogo nilikaribia kuupoteza ubingwa walonipa hao mabibi na mabwana nilipoelekea chuo kikuu nchini Kenya na Marekani, walakin kazi yangu ya uandishi habari ilizidi kunikumbusha kitambo kile kitamu:-)
Pia nawashukuru marafiki zangu toka Kenya na Tanzania ambao, kwa bidii yao katika kutunza usanifu wa lugha hii tukufu, wamenitia moyo kuzingatia mwendo huu.
Mwisho, nawashukuru wazee wangu ambao – tofauti kabisa na Wakenya wengi – wazingatia umuhimu wa kuzungumza na kuandika Kiswahili sanifu.
Blogu hii itawapeni habari zote nitakazochapisha kwenye ile blogu yangu ya Kiingereza, yaani Kenyananalyst.
Ni matumaini yangu kuwa sitowanyimeni ukweli na utamu mnaostahili kwa kuwa wasomaji wangu waaminifu katika lugha hii “mpya” namna mlivyokuwa upande wa pili.
Karibuni tena na Mungu awabariki!
Mwenzenu,
Yesse.

Advertisements

Entry filed under: Uncategorized.

“A planetary event is going to take place above the Earth” The True Hero of the Titanic

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Kenyan Analyst

Recent Posts

April 2006
S M T W T F S
« Mar   May »
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
30  

Feeds


%d bloggers like this: