Utamu wa kuzungumza na ndugu Mtanzania

December 5, 2006 at 5:31 pm 3 comments

Leo asubuhi nilipata nafasi kuzungumza na rafiki yangu mmoja toka Tanzania.  Huu hapa mukhtasari wa mazungumzo yetu.

MIMI: Ah kamanda, za siku nyingi?
YEYE:  Salama kabisa mkubwa.  Habari ya huko
MIMI: Mwenzako sijambo. Nashukuru tu.  Sijui wewe?
YEYE: Hata huku mambo ni mazuri kabisa ndugu.  Vipi mradi wenu, unaendeleaje?
MIMI: Uhhmn.  Mradi upi – nikumbushe kidogo hapo.

YEYE: Wa Mzalendo au wewe huhusiki nao?
MIMI: Oh, huo.  Sihusiki, ingawa wanaofanya hayo ni wanablogu wenzangu.
YEYE: Ok. Na ule wa KBW?
MIMI: Ule wa KBW – mimi ni member / mhusika; sihusiki na usimamizi wake kwa namna yoyote ile.
YEYE: Ok.  Mmepiga hatua wenzetu hata hivyo.  Sisi ndio kwanza tunajikongoja kuunda jumuiya.
MIMI: Ninafwatilia kwa karibu mijadala ambayo mmekuwa nayo siku za hivi karibuni.  Nafurahishwa sana na bidii na ukakamavu wenu.  Ndugu Jikomboe amekuwa akitupasha habari kupitia blogi yake.
YEYE: Tunajitahidi sana ila mgongano wa kimawazo ni mkubwa sana.
MIMI: Mgongano? Yaani wamaanisha tofauti za kimtazamo?
YEYE: Lakini nadhani ni vyema kukawa na mgongano wa mawazo wa namna hiyo sababu mkifanikiwa kuudhibiti na kuunda Jumuiya hiyo mnakuwa na kitu madhubuti sana.
MIMI: Kweli kabisa.  Vipi habari za Richmond na umeme  Nazisoma magazetini tu.
YEYE: Usanii wa hali ya juu kamanda.  Simulizi za umeme zinatia kinyaa kuzisikia yaani hata magazeti siku yakiandika habari za umeme hayauziki siku hiyo huwezi amini.
MIMI: Mvua ilianza kuwapigia wapi?  I mean – kuwanyea.
YEYE: Unajua serikali hii ilikuja na ahadi nyingi sana, haikuwa na vipaumbele katika kukabiliana na matatizo ya wananchi na haya ndio matokeo yake, yaani wanataka kufanya kila jambo kwa wakati mmoja, barabara, umeme, maji, shule, chakula, kilimo n.k.
MIMI: Uhhmn, pupa, eh!
YEYE: Sasa inakuwa ngumu, wamejikuta wameshindwa sasa, ndio maana hata jamaa wanawachezea kila siku, leo wanaingiza mtambo mnategemea kuwa ahueni inakuja kumbe kesho wanatangaza tena kuongezeka kwa masaa ya mgao wa umeme.
MIMI: Uchungu ulioje hapo. Na je, yale majibwa ya upinzani yasemaje?  Hayana makali bado, eh!
YEYE: Wamekaa kimya tu.  Hawajui hata waanzie wapi kusema nadhani, japo kwa hali ilivyo hata wakisema inakuwa kazi bure.  Hata vyombo vya habari wajua haviwapi uzito siku hizi, vilishamwingiza jamaa madarakani sasa haviwezi hata kufanya assesment na kumkosoa.
MIMI: Wajua, hivyo ndivyo mambo yalivyokuwa huku kwetu.
YEYE: Yeah, nakumbuka
MIMI: Vyombo vya habari, haswa kundi fulani hapa, lilisaidia upinzani kuingia maradakani kwa kiasi kikubwa.
YEYE: Matokeo yake ndio wanashindwa hata kumnyooshea kidole sasa, maana wanaogopa kusutwa na wananchi kuwa waliwadanganya.

MIMI: Upande wa pili, kuna kundi la lingine ambalo kabla ya Kibaki, lilimpa mkono wa msaada mzee Moi sana.  Tangu 2003, kundi hili limejitwika jukumu la kumkosoa Kibaki, kiasi cha kumkera sana wakati mwingine.  Na kadri siasa za Kenya zinavyochukua mwelekeo na mkengeuko mpya kila kukicha, ndivyo pia vyombo vya habari vinajibadili hapa na pale.
YEYE: Lakini wanachosema si kweli?
MIMI: Ukweli upo hapa na pale.
YEYE: Kinachotatiza huku kwetu ni kuwa kila gazeti lilikuwa upande wa JK, kiasi kwamba hadi sasa hakuna linaloweza kuthubutu kumnyooshea kidole.  Hata Free Media ambayo ni ya Mbowe, aliyekodi helikopta huko kwa ajili ya kampeni hawawezi kusema kitu ati.
MIMI: Ah, Mbowe alikodi ndege ya yule bwana Nyachae, mmoja wa mabwenyenye wa Kenya.  Na Reginald Mengi je? Hamna sauti huko?
YEYE: Huyo ndio kabisaaa kabakia kujiandika miradi yake mwenyewe kwenye vyombo vyake
MIMI: Debe tupu hutika sana, wajua tena
YEYE: Ndio ilivyo.  Wanaenda nje leo wanaahidiwa mvua za kupandikiza, wanakuja wanatutangazia meno yote nje, wanatuona wajinga sana kiasi kwamba hatuwezi hata kuchambua gharama za miradi kama hiyo.  Wao wanachekelea tu sababu wanajua lazima kuna 10% kwenye ulaji kama huo.
MIMI: Wanikumbusha sana yule bwana, – Hussein Mohammed.
YEYE: Leo wameenda sijui wapi huko wameahidiwa umeme wa upepo, wanachekelea tu, hatujasikia wakikusanya wataalamu wa humu nchini kujua kama unawezekana na gharama yake itakuwa na madhara gani kwa uchumi wa nchi.
MIMI: Yeye na pia Mohammed Said Mohammed bila ya kumsahau Shaaban bin Robert na wenzao.  Falsafa yako iko pale pale nao, – kuwa uongo wa wengi wanaotawala barani Afrika umekithiri kiasi cha haja.
YEYE: Kwakweli.  Wajua mie nimesomea mazingira, na hata uandishi wangu ni wa mazingira zaidi huku kwenye siasa nilijiingiza tu basi sababu ni sehemu ya maisha
MIMI: Uhmn.
YEYE: Hivi wanawezaje kutuambia kuwa wanaweza kunyunyiza mawingu Mtera kisha mvua inanyesha pale wakati Mtera iko ukanda wa kati ambako kuna upepo pengine kuliko sehemu zingine za nchi?
MIMI: We bwana wasahau upesi kuwa miujiza hufanyika Afrika? 🙂
YEYE: Duh!! Huenda sisi ndio tungekuwa wa kwanza. Kuna mradi wa maporomoko ya maji mahali Iringa, ulishafanyiwa upembuzi toka miaka ya 70, umeachwa hadi leo hii wanatuletea habari za mvua za kupandikiza na umeme wa upepo.
MIMI: Ha! Ha! Ha!
YEYE: Huko kwenyewe wanakouchukulia huo ujuzi hawatumii huduma hizo kama za msingi bali za dharura tu.
MIMI: Ndiyo mojawapo ya maajabu ya bara letu.  Sijui iwapo wamkumbuka Karama?
YEYE: Sijui tutaendelea lini kwakweli.  Karama yupi?
MIMI: Karama – Yule mhusika mkuu kwenye diwani ya Shaaban bin Robert – KUSADIKIKA?
YEYE: Yeah, namkumbuka na mikasa yake
MIMI: Zaidi ya hiyo mikasa, kulikuwa na wasifu tatu.  Wasifu ulomtofautisha na waziri mkuu.
YEYE: Wajua tungekuwa na watu wenye mawazo ya akina Shaaban Robert kama kumi tu hapa duniani, wakatiwa chache na akina Nyerere, Mandela na Samora kama kumi nao, dunia ingekuwa nchi ya ahadi.
MIMI: Umenena kweli.  Karama – Alikuwa na bongo la hekima, moyo wa ushujaa, na ulimi wa nasaha. Hizo ni baadhi ya wasifu ambao kiongozi afaa kuwa nazo.
YEYE: Viongozi wetu wa sasa pia wana sifa hizo.   Wana Bongo za wizi, Moyo wa kutetea maovu na uonevu, na Ndimi za unafiki kwa kiwango kisichomithilika.
MIMI: Mcheshi wewe!
YEYE: ndio hali halisi.  Wajua saa zingine mtu unaweza kujiuliza hivi kwanini ulizaliwa sehemu kama hii?  Lakini baadaye unajijibu kuwa Mungu alikuwa na sababu zake kukufanya uzaliwe mahali kama hapo, kwa maana wewe ndiye unatakiwa kupiga kelele kubadili hiyo hali
MIMI: Kweli kabisa.  Ajabu ni kuwa licha ya tofauti zetu za kidini, tuna uwiano mkubwa wa kimaantiki hapa.  Una bongo zuri ndugu.
YEYE: Ukiangalia sana viongozi wetu sasa wanasifia mashujaa waliokuwepo awali, lakini hawafanyi jitihada zozote katika kutengeneza mashujaa wa kesho au keshokutwa, na hili likimaanisha kuwa wanawekeza katika kuua mataifa yao.  Wanapalilia mazingira ya ukoloni mwingine siku zijazo
MIMI: Ukoloni mamboleo – hiyo ni injili kama ilivyoandikwa na Hussein.  Nakubaliana nawe.
YEYE: Wanajenga mazingira na madaraja baina ya waliosoma na kubahatika kwenda nje na wale wasiojua chochote, matokeo yake wanaoitwa wasomi wetu ndio hao wamekuwa wakiingia mikataba ambayo inawaumiza wananchi kila kukicha na ikifika wakati masikini ambao hata hawakusaini mikataba hiyo wameshindwa kujikamua ili kulipia madeni ya wapuuzi wachache waliosaini mikataba ya kilaghai, ndio hapo nchi nayo itabinafsishwa
MIMI: Mwandishi Achebe, katika kitabu chake THE TROUBLE WITH NIGERIA, asema kuwa viongozi wa aina hiyo ndio wanaonajisi nchi zao kisiasa, kijamii na kiuchumi kisha wanapozungumza hadharani, wazisifia nchi zao kwa kusema “taifa letu tukufu.”  Ni kinaya kilichoje.  Wao ndiyo wanaamua ni nani atakuwa mzalendo na kwa kigezo cha aina gani.  Kimsingi, ni maoni yangu kuwa itabidi kizazi chenu kizingatie hatima ya TZ zaidi na baada ya JK.  Na siyo JK tu, ila pia wote ambao ni viongozi kwa wakati huu.  Na hiyo ni changamoto iliyo mbele ya kila taifa barani Afrika.
YEYE: Kweli kabisa.  Nitakukimbia baada ya muda kidogo kamanda
MIMI: Sawa ndugu.
YEYE: Nadhani tunaweza kuwasiliana baadae tena kama muda utapatikana
MIMI: Nashukuru kwa gumzo ambayo tumekuwa nayo.  Nimefurahi sana.

YEYE: Salamu kwa ndugu zangu wote wa ulimwengu wa blogi nchini Kenya.  Najua ipo siku mtafanya mapinduzi makubwa sana.
MIMI: XXXXXXXXXX ndiyo namba yangu iwapo utajipata Kenya wakati wowote.  Mapinduzi yaja kwa wakati wake.

Advertisements

Entry filed under: Africa, Culture, Economics, Humour, Kenya, Literature, Media, Politics, Religion, Science, Society, World.

Though clergymen disappoint, Nativity story doesn’t Jenkins’ latest thoughts on global Christianity

3 Comments Add your own

 • 1. larrymads  |  December 6, 2006 at 3:34 pm

  Ingawa nilisoma tu labda nusu peke yake ya mazungumzo yenu, nilioenelea ipo haja kubwa ya kutafsiri mnachoongelea maana wengi(ne) wetu hatukuelewa. Waandishi wa magazeti wa huko kweli wana kibarua kigumu kujulisha taifa lote habari kwa Kiswahili. Kwnagu mimi ni kuwatakia mema. Naelewa kwa nini hata huku kwetu wameanza kujaajaa (Swaleh na wenzake kwenye vyumba vya habari vya Kenya). Mimi naomba kutia kikomo hapo hadi wakati mwingine.

  Reply
 • 2. KA  |  December 6, 2006 at 4:22 pm

  Ah, Larry, usimtie aibu mwalimu wako wa lugha na fasihi katika Kiswahili 🙂 Hata hivyo, umejribu zaidi ya Mkenya wa kawaida 🙂

  Reply
 • 3. galasha  |  March 7, 2008 at 8:11 am

  kwa kweli mazungumzo yenu yamenivutia hasa pale kuhusu mvua za upepo. Yule aliyekuwa ameahidiwa hayuko madarakani tena vile vile mkosa wa wale waliokuwa wanatarajiwa kuleta mvua za upepo nao serikali yao iliangushwa. Mkosi kweli kweli.

  Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Kenyan Analyst

Recent Posts

December 2006
S M T W T F S
« Nov   Jan »
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  

Feeds


%d bloggers like this: