Azimio la semina elekezi ya Ibilisi

April 8, 2007 at 10:42 pm 4 comments

*Mmoja wa marafiki zangu toka nchi jirani yaTanzania amenitumia ujumbe ufwatao. Ni tafsiri ya barua ambayo huenda baadhi yenu mshapokea kimbele.

Shalom,

Habari za ubusy?
Naamini unaendelea kuitafuna vyema pasaka yako na familia yako. Ninaamini hiki ndio kipindi pekee wewe hauko busy sana lakini kuanzia jumanne ubusy wako utarudi kutoka mapumzikoni kabla haujarudi sikiliza hii.


“Baada ya semina elekezi kwa viongozi na watumishi wa Serekali
iliyofanyika huko Ngurdoto mkoani Arusha iliyoongozwa na rais Jakaya
Mrisho Kwikwete, na baadae semini nyingine elekezi zilizofwatia baada
ya hapo kama ile ya mkuu wa mkoa wa Arusha kwa watendaji naviongozi
mbalimbali wa mkoa wa Arusha na nyingine kama hizo katika mikoa
mingine Tanzania.

Shetani naye aliitisha semina elekezi kwa mapepo
duniani na katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo
alisema”Tumeshindwa kuwazuia wakristo wasiende kanisani””Tumeshindwa
kuwazuia wasisome biblia zao na kufahamu ukweli””Tumeshindwa hata
kuwazuia wasiwe na mapenzi ya kwelikwa Mwokozi wao” “Mara wapatapo
muungano wa kweli na kristo, mamlaka yetu yatakuwa yamefika
mwisho.””Kwahiyo waacheni waende kanisani, waacheni waendelee na
karamu zao za upendo, LAKINI waibieni muda, iliwasipate nafasi ya
kudumisha mahusiano na mapenzi yakweli kwa Yesu Kristo….” “Hiki
ndicho ninachotaka mfanye.” alisema Shetani:”wataabisheni wasipate
kamwe kushikamana na mwokozi wao na wasifungamane naye kwa siku
nzima!” “tutafanyaje jambo hilo?” Mapepo
yalimwuuliza kwa jazba.
“hakikisheni wanakuwa ‘BUSY’ (BUSY= Being Under Satan’s York) katika
mambo yasiyokuwa na umuhimu katika maisha yao na muanzishe mipango
mingi sana isiyohesabika ili kujaza akili na ufahamu wao,”alijibu
shetani “wapeni kutumia, na kutumia, na kutumia; na kukopa, nakukopa,
na kukopa.” ‘washawishini wake zao waende kufanya kazi kwa siku
kushinda huko kwa masaa mengi sana kwa siku na waume zao wafanye kazi
kwa siku sita hadi saba kwa wiki, na masaa 10 hadi 12 kwa siku, ili
wasiweze kupata nafasi ya kutulia na kutafakari chochote kulingana na
mfumo huo wa maisha.” “Wazuieni wasiwe na nafasi ya kukaa na watoto
wao” “Familia zao zikiparaganyika, mara, nyumba zao hazitakwepa
msongamano wa kazi na mawazo.” “Wachocheeni zaidi akili na fahamu zao
ili kuhakikisha kwamba hawaiskii ile
sauti ndogo, tulivu ya Mungu
wao.” “Washawishini walize radio au kaseti au muziki kwenye
simu,popote wanapoendesha gari au wanapotembea kwa miguu .” waache TV,
VCR, CD na KOMPYUTER zikiwa zimewashwa kama kawaida majumbani mwao na
mhakikishe kwamba kila duka na mgahawa kote duniani linapiga muziki
usiokuwa wa kibiblia mfululizo bila kukoma.” “Hii itasonga akili na
fahamu zao na kuvunja ule muungano wa Kristo.” “Jazeni magazeti na
vijarida mbalimbali kwenye meza zao za kahawa na chai dunia kote.”
“Shindilieni habari na matukio mbalimbali ndani yafahamu zao kwa muda
wa masaa 24.” “Ingilieni kwenye muda wao wa kuendesha barabarani kwa
kuwaonyesha mabango na matangazo.’ “Kwenye masanduku ya postana barua
pepe jazeni vipeperushi na majarida na kila aina ya matangazo yahabari
za vitu na hudumu
yanayowapa matumaini ya uongo.” “Wekeni wanawake
warembo sana mitaani na kwenyeTelevisheni na majarida ili kwamba
wanaume walioko kwenye ndoa wadanganyike na kuamini kwamba urembo
wanje ndio muhimu, na wasiridhike na wake zao.” “wafanye wake zao
wachoke sana wasiweze kuonesha upendo kwa waume zao usiku.” ‘Wapeni
maumivu ya kichwa pia!” “kama hawatawapa waume zao upendo
wanaouhitaji sana,wataanza kutazama kwingine.” “Hiyo itaparaganyisha
familia zao haraka sana!” “wapeni waalimu wa uongo ili wawapotoshe
wasifundishe injili ya kweli kwa watoto wao na waumini wao.” “Wapeni
zawadi na kadi za pasaka ili wasizungumzie nguvu za ufufuka kwa Kristo
juu ya dhambi na mauti.” “Hata katika karamu zao wachosheni sana kwa
anasa nakuwafanya warudi wakiwa wamechoka
sana.” “Hakikisheni
wanakuwa ‘BUSY’ na kusongwa na mambo kiasi kwamba hawapati muda wa
kutafakari wema wa Mungu. Badala yake wapeni kutalii kwenye maeneo ya
ajabu,matukio ya michezo, matamasha, kumbi za sinema na video.
“Wafanye wawe ‘BUSY,’ ‘BUSY,’ ‘BUSY,! Yaani wasongwe na kusongwa na
kusongwa na kazi kwelikweli!” “Na wanapokutanika kwenye ibada zao za
kiroho wafanye waingie katika umbea na fitina na kuzungumzia mambo
madogo madogo ya umbea na fitina ili waondoke wakiwa na dhamira mbaya
zilizochafuliwa.” “Jazeni visababishi vingi vya mambo katika maisha
yao ili wasiwe na nafasi ya kutafuta msaada na nguvu za Yesu.” “Muda
si mrefu watakuwa wakitegemea akili zao wenyewe,wakihatarisha afya zao
na za familia zao kwa ajili ya maangamizi yao wenyewe.” “Itafanya

kazi” “Itafanya kazi!”Huu ni mkakati kweli kweli !Mapepo yaliondoka
kwenye mkutano yakiwa na hamu kubwa sana ya kutekeleza majuku hayo
waliyopewa na kuanza kuwafanya wakristo wawe na kukimbia na mambo huku
na huko.wakawa na muda mdogo sana kwa ajili ya Mungu wao na familia
zao.Wakakosa muda wa kuwaeleza wengine kuhusu nguvu za Yesu kristo
kubadili maisha ya wanadamu.NADHANI SWALI NI JE SHETANI AMEFANIKIWA
KATIKA MIPANGOYAKEHIYO?WEWE NDIYE HAKIMU!!!!!!!!!!je ‘UBIZE’ au
kutingwa na kazi kunamaanisha : kuwa chini ya mkataba au utumwa wa
shetani?
WAfahamishe wengine uwapendao na dumu katika KRISTO YESU aliye tumaini na mkombozi wetu.

PASAKA NJEMA!!!

Advertisements

Entry filed under: Africa, Culture, Economics, Kenya, Literature, Media, Missions, Personals, Prophecy, Religion, Science, Society, World.

Radical Effects of the Resurrection “I have heard it too, the quakes will come!”

4 Comments Add your own

 • 1. thelamp  |  April 9, 2007 at 12:12 am

  please go to http://thelamp.wordpress.com/2007/04/08/what-does-god-have-to-say/

  Reply
 • 2. toiyoi  |  April 9, 2007 at 7:29 pm

  KA,
  Thanks for the message.
  PS: whats up with that BIG RED font. rather uncomfortable to read

  Reply
 • 3. Eddy Albert  |  May 20, 2007 at 4:44 pm

  Naomba muchangie kujadili mada hii inayohusu maneno ya G. A. Buttrick katika kitabu chake cha The Interperters Dictionary Of The Bible katika “Text, NT” Vol. 4 asema: “The NT (new testament) is now known, whole or in part in nearly five thousand Greek MSS (manuscripts) alone. Every one of these handwritten copies differ from every other one.. it is safe to say that there is not one sentence in the NT in which the MS tradition is wholly uniform…… many of them do have theological significance and were introduced into the text intentionally”; ni mimi sijaelewa, au ni yeye amekosea, au ni kweli aliosema? Itakuaje kitabu kama hichi cha kueleza Kitabu kitakatifu kieleze maneno kama haya? Au si kitabu cha kutegemewa hivo? na maneno aliosema si sawa? Bora iwe hivo; maanake yaweza kuwa hata hivi vitabu vitakatifu vinavotumiwa vina makosa?!!! naomba majibu na mchango wenu kwa ajili nina masuali mengi sana yanayonitatiza.

  Reply
 • 4. Eddy Albert  |  May 20, 2007 at 5:28 pm

  mbona sijapata jawabu? ni muhimu sana!

  Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

Trackback this post  |  Subscribe to the comments via RSS Feed


Kenyan Analyst

Recent Posts

April 2007
S M T W T F S
« Mar   May »
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930  

Feeds


%d bloggers like this: